"Hali ya Q Chief si Salama Anahitaji Msaada Mkubwa Sana"..Mke Afunguka


Mke wa msanii wa muziki wa bongo fleva Q Chief, anayejulikana kwa jina la Eliza, amesema kwamba mume wake anahitaji msaada zaidi, kwani hayuko sawa.


Eliza ameyasema hayo alipokuwa akizungumza kwenye Friday Night Live ya East Africa Television, na kusema kwamba mume wake huyo ambaye kwa sasa wametangana, anaonekana hayuko sawa kwani amemfanyia vurugu na kumtolea maneno machafu, hivyo ni vyema iwapo atapatiwa msaada.

“Katoka kunifanyia vurugu saa hivi, kanitukana sana, kuna makosa amefanya lakini siwezi kuongea, hata aibu kuongea, kuna vitu alikosea akaondoka mwenyewe, ameamua mwenyewe hakufukuzwa, sasa ndio maisha ambayo amepanga, kasema anaacha muziki amemrudia Mwenyezi Mungu ambapo ni suala jema, ila hayupo normal, anahitaji msaada”, amesema Eliza.

Msanii huyo hivi karibuni ametangaza kuachana na muziki, huku akijilaumu kuwa amekosea sana familia yake na watoto wake na mke wake kumkimbia, hadi kufikia kutoa machozi mbele ya waandishi wa habari. 

0 Comments

Previous Post Next Post