FREEMAN Mbowe 'Imeniwia Vigumu Sana Kumpa Pole Mbunge Heche Kwa Kifo cha Mdogo Wake'.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amefunguka na kusema kuwa kwa siku kadhaa zilizopita amekuwa katika wakati mgumu na kushindwa kuelewa neno gani anaweza kumpa Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini, John Heche kufuatia kifo cha mdogo wake Suguta ambaye alifariki kwa kuchomwa kisu na askari

 Mbowe amesema kuwa kifo ambacho kilimpata mdogo wake na Heche kinaumiza sana ndiyo maana kwa siku kadhaa amekosa maneno mazuri ya faraja kumpa kiongozi huyo wa CHADEMA

"Ni siku ya 3 sasa toka ulimpozika mdogo wako, nimefikiria kwa muda mrefu, maneno gani nitumie kukupa pole lakini imeniwia vigumu sana kuyapata maneno hayo kutokana na aina ya kifo kilichokatisha maisha ya kijana mdogo kabisa katika Taifa. Tunafundishwa ya kwamba tushurukuru kwa yote,liwe baya au zuri, sawa tunashukuru lakini kwa kifo cha aina ya mdogo wako kinauma na kuumiza sana, bora mtu akiumwa inakuwa ni rahisi mnasema ni kazi yake Mungu hakuna anayeweza kuipinga na huwa ni kipindi kigumu kuliko wakati mwingine wote wote katika maisha yetu wanadamu pale tunapoondokewa na wapendwa wetu lakini kwa kifo cha aina ya mdogo wako ni maumivu zaidi" 

Aidha Mbowe alitumia wakati huo kutoa pole kwa familia ya John Heche kufuatia kifo cha mdogo wake huyo

"Nakupa pole sana Kamanda Heche John katika kipindi hiki kigumu, Mungu akupe nguvu wewe, familia, ndugu, jamaa na marafiki, pole kwa mara nyingine kamanda, apumzike kwa Amani Kamanda Suguta"

0 Comments

Previous Post Next Post