Ebitoke Ashindwa Kumuelewa Shilole " Mi najua ni Mpishi Tu"

Ebitoke Ashindwa Kumuelewa Shilole " Mi najua ni Mpishi Tu"

Mchekeshaji maarufu wa kike nchini Tanzania, Ebitoke ameshindwa kuelewa kama Shilole ni msanii wa muziki au muigizaji kwani hafahamu hata kazi moja ya sanaa ambayo mrembo huyo alishawahi kuifanya zaidi ya kazi yake ya mama ntilie anayoifanya kwa sasa.

Ebitoke amesema hayo leo kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV, alipotakiwa na moja ya wafuatiliaji wa kipindi hicho ataje wimbo japo mmoja wa msanii huyo wa Bongo Fleva na kuuimba.

“Labda unitajie nyimbo zake mimi sizijui kazi zake, mimi najuaga yeye ni mpishi tu ila kwenye nyimbo hapa mtanisamehe sijui nyimbo zake.. Nisiwe muongo naongea ukweli na sio kiki kama mlivyozoea mambo ya kiki siku hizi nimeacha.“amesema Ebitoke.

Kwa upande mwingine Ebitoke amesema kuwa watu wengi wanamuona mchekeshaji lakini hiyo sio kazi anayoipenda katika maisha yake anapenda kuwa muigizaji na ndoto yake kubwa ni kuja kushinda tuzo ya Oscar ili kuitangaza zaidi Tanzania .

Shilole ni muigizaji wa kwanza kuacha fani hiyo na kukimbilia kwenye muziki ambapo tangu aingie ametoa nyimbo kibao kama Nakomaa na jiji, Kigori, Lawama, chuna buzi na nyingine nyingi. 

0 Comments

Previous Post Next Post