Diamond Sheik Kipozeo Wazindua Kipindi cha 'Nyumba ya Imani' cha Wasafi TV

Diamond Sheik Kipozeo Wazindua Kipindi cha 'Nyumba ya Imani' cha Wasafi TV

MKALI wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’,  na Shekhe maarufu jijini Dar, Shekhe Kipozeo, usiku wa kuamkia leo walishirikiana kuzindua kipindi kipya cha runinga kinachojulikana kwa jina la Nyumba ya Imani, ambacho kitakuwa kikirushwa kila siku ndani ya Wasafi TV.

Uzinduzi huo ulioambatana na futari, ulifanyika katika jengo la ofisi za Wasafi TV, zilizopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, ambapo Shekhe Kipozeo alipewa heshima ya kuzindua kipindi hicho kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa runinga hiyo, Diamond Platnumz.

“Tunafurahia leo kuwaona wapendwa wetu mmetuunga mkono katika kufanikisha kipindi chetu hiki kipya, ni matumaini yangu kila mmoja amekuja kwa mapenzi yake na kwamba tutaendelea kushirikiana kwa kila jambo letu kwani TV hii ni yetu sote,” alisema Diamond.

0 Comments

Previous Post Next Post