City Wamebeba Ubingwa Lakini United Watapewa Pesa Nyingi Kuliko Wao,Sababu ni hii.


Msimu wa EPL 2017/2018 unakwisha rasmi Jumapili ya jana, na mabingwa wameshapatikana ni Manchestwe City huku pia timu zinazoshuka daraja zimeshajulikana ni Stoke City, Swansea na West Bromich Albion.

Kushinda kwa Manchester City kunamaanisha watapewa £153.2m kutoka PL, pesa hizi ni kutokana na namna ambavyo mechi zao zimerushwa na pia kuna kiasi cha pesa ambacho timu zote za EPL hupewa.

Iko hivi City kama bingwa napewa £39.8m kutoka Epl, lakini pia kuna hii pesa ambayo kila timu wanapewa kiasi sawa(equal share) ambapo huwa ni £82m, pia kuna pesa kutokana na idadi ya mechi zako zilizooneshwa live(haki kutoka Epl) na hii walitakiwa kulipwa £31.5m, jumla ya pesa zote hizi ni £153.2m.

Sasa linapokuja suala la United wao japo wamemaliza nafasi ya pili lakini watapewa pesa kuliko bingwa, United watapokea £153.6 kwanini? Baasi ni hivi United wanapokea kama kawaida equal share ya £82m, wakati City anapokea £39.8m za ubingwa, United wanapokea £37.8m ya mshindi wa pili, lakini United mechi zao ambazo PL walirusha hewani live ni mechi mbili zaidi ya City na hii imewapa £33.9m katika mechi hizo na hapa ndipo walipowaacha City.

Suala hili lipo pia kwa mshindi wa 3 na wa 4, Tottenham amemaliza ligi katika nafasi ya 3 lakini jumla ya pesa ambayo wamevuna ni kiasi cha £148.1m, hii ni pesa ndogo kuliko ambayo Liverpool ambao wamemaliza ligi katika nafasi ya 4 wamevuna, Liverpool wamepata £149.6m na hii ni kutokana na mechi zilizoenda live.

Vilabu vilivyoshuka daraja navyo sii haba kwani wameshuka na fungu kubwa la pesa, Swansea amevuna £100m, West Bromich wakiweka mfukoni kiasi cha £98.5m sawa na mshindi wa mwisho Stoke City na hii imechagizwa sana na hii pesa £82.0m ambayo EPL wamekuwa wakitoa kwa kila timu. 

0 Comments

Previous Post Next Post