Breaking News: Maafisa Watatu wa TIC Wafariki Dunia Kwenye Ajali ya Gari

Breaking News: Maafisa Watatu wa TIC Wafariki Dunia Kwenye Ajali ya Gari

MAOFISA watatu wa Kituo cha Uwekezaji cha nchini  (Tanzania Investment Center (TIC) wamefariki dunia katika  ajali ya gari usiku wa kuamkia leo maeneo ya Chalinze wakiwa njiani kuelekea jijini Dodoma.


Waliofariki ni Saidi Amiri Moshi (Kaimu Mkurugenzi wa Research zamani Corporate Affairs), Zacharia Kingu (Kaimu Mkurugenzi wa Corporate Affairs zamani Investment Promotion) na Martin Masalu (Meneja Research).


Waliopata majeraha ni wawili yaani Godfrey Kilolo (Meneja wa Sheria) na dereva wa gari hilo aliyejulikana kwa jina moja tu la Priscus. Wote walikuwa wakielekea Dodoma kwa ajili ya mkutano ambao unatakiwa kufanyika leo Jumanne jijini humo.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo. 

0 Comments

Previous Post Next Post