Bodi ya Ligi Yamsimamisha Kelvin Yondani Kuchezea Yanga.


Bodi ya Ligi Tanzania, imetangaza kumsimamisha beki wa Yanga, Kelvin Yondani kutokana na kuonekana katika video akimtemea mate beki, Asante Kwasi.

Mtendani wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amezungumza hivi punde na kusema suala lake limepelekwa Kamati ya nidhamu baada ya kuonekana haliwezi kusikilizwa na Kamati ya Saa 72 iliyokaa.

"Kwa hiyo sasa tunamsimamisha hadi hapo kamati itakapokaa na kuamua kuhusiana na suala lake," alisema Wambura.

Katika picha ya video ilimuonyesha Yondani akimtemea Kwasi raia wa Ghana katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyowakutanisha watani wa jadi, Yanga na Simba ambao walishinda kwa bao 1-0.

Suala hilo lilizua mjadala mkubwa miongoni mwa wadau, wakiwemo waliomtetea Yondani na walioona haikuwa sahihi.

0 Comments

Previous Post Next Post