Bill Nass Afunguka Kuhusu Picha Zake Zinazosambaa Mtandaoni.


Rapa Billnass ambaye anatamba na ngoma ya 'Tagi Ubavu' amefunguka na kudai kipindi hiki kigumu anachokipitia kwa watu kuweka picha zake mitandaoni zikiwa zinamzungumzia ndivyo sivyo zinampa nafasi kubwa ya yeye kuwajua watu zaidi jinsi akili zao zilivyo katika kutafakari baadhi ya mambo.


Billnass amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI baada ya kuulizwa swali na muongozaji wa kipindi hicho Elbogast Myaluko kama alipata bahati ya kukutana na picha yake mitandaoni aliyopiga kwenye hafla ya harusi ya Alikiba siku za hivi karibuni iliyokuwa ikisambazwa na mashabiki zake ikiwa na ishara kama anakanda unga hivi.

"Ni kweli nimekutana nayo hiyo picha, lakini haipo kama watu wanavyoizungumzia na kuonekana, ile picha nilipigwa wakati nilikuwa naongea na mtu. Kwa bahati mbaya mimi nikiwa naongea huwa natumia ishara ya vitendo kwa sana, na pale nilipokuwepo palikuwa na kelele sana. Kwa hiyo sijui nilipigwa muda gani lakini watu waliikata nikaanza kuiona twitter", amesema Billnass.

Pamoja na hayo, Billnass ameendelea kwa kusema "kila mtu na akili yake unajua kuna watu wengine wewe unapomaliza kufikilia wao ndio wanaanza kwa hiyo kila mtu ana mpaka wake wa mawazo. Niliona lakini nikaona siwezi kujibizana na kila mtu. Haiwezi kuniumiza ila napata nafasi ya kuwajua watu zaidi jinsi walivyo". 

0 Comments

Previous Post Next Post