BILL NASS ADAI ANAKUTANA NA NANDY POLISI TU


Msanii Bill Nass amesema tangu ilipovuja video yake ya faragha akiwa na Nandy, wamekutana mara moja tu.

Hata hivyo hilo halimaanishi kuna kitu hakipo sawa kati yao, hapana!, wao bado ni marafiki na kilichotokea ni sehemu ya kujifunza.

“Tangu niliporudi nimeonana na Nandy mara moja tu, siku tulipoenda polisi kutoa maelezo nini kimetokea, nilizungumza nae tu kutaka kufahamu kuhusiana na kesi iliyopo polisi,” amesema.

“Nandy ni rafiki yangu, yaliyopita ni sehemu ya kujifunza maisha na kuhakikisha huko mbele jambo hili halijitokezi tena,” Bill Nass ameiambia XXL, Clouds FM.

Bill Nass ameongeza kuwa polisi bado wanaendelea na uchunguzi ili kubaini ni nani aliyesambaza hiyo video.

0 Comments

Previous Post Next Post