BILA MAPUMZIKO YANGA KUELEKEA MBEYA LEO,KUHUSU HALI ZA WACHEZAJI KIAFYA,MAMBO YAKO HIVI.


Na George Mganga

Kikosi cha Yanga kinaondoka jijini Dar es Salaam leo Jumatano kuelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa kesho Alhamis kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya.

Bila mapumziko, kikosi hicho kinaunganisha safari hiyo leo baada ya kuwasili jana nchini kikitokea Algeria kushiriki mashindano ya kimataifa.

Yanga ilikuwa Algeria mjini Algiers kwa ajili ya mechi dhidi ya USM Algeri iliyochezwa kwenye Uwanja wa Julai 5, 1962 na kupoteza kwa mabao 4-0.

Tanzania Prisons watakuwa wanaikaribisha Yanga ambayo dalili zinaonesha tayari ubingwa ilishauweka rehani kutokana na watani zao wa jadi Simba kuhitaji alama moja pekee ili watangazwe kuwa mabingwa.


Taarifa zinaelezwa kuwa wachezaji wote waliokuwa wamesafiri hali zao kiafya zinaendelea vizuri na wako tayari kwa safari ya Mbeya.

0 Comments

Previous Post Next Post