Barakah The Prince Afunguka Ishu ya Kusaini WCB.


Msanii wa muziki Bongo, Barakah The Prince amefunguka kuhusu tetesi za kujiunga na label wa WCB.

Muimbaji huyo ameiambia Rick Media kuwa WCB ni kama familia yake ila suala la kujiunga na label hiyo halina ukweli wowote.

“Hapana, WCB ni kama familia yangu, mara nyingi hata mameneja wa WCB ndio wanakuwa wananiongoza na kunielekeza nifanye nini,” amesema Barakah.

“Kwa hiyo tumeamua kuwa kama familia na kuna wasanii wengi wanafanya vizuri, lakini sio kwamba nipo chini ya WCB, no siyo kweli,” amesisitiza.

April 25, 2018 Dj wa Diamond Platnumz ‘Romy Jones/Rj The Dj’ aliachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Bora Iwe akiwa amemshirikisha Baraka The Prince.

Utakumbuka July 21, 2017 Baraka The Prince alitangaza kuondoka katika label ya Rockstar4000 kwa kile alichodai kuna mambo hayapo sawa kati yake na menejimenti hiyo. 

0 Comments

Previous Post Next Post