Aliyepasuliwa Kichwa Badala ya Mguu Kulipwa Milioni 100.

Aliyepasuliwa Kichwa Badala ya Mguu Kulipwa Milioni 100

Mahakama Kuu imeamuru Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu ya MOI kumlipa fidia ya Milioni 100 Emmanuel Didas aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa badala ya mguu kutokana na madhara aliyoyapata ya kimwili na kiufahamu ikiwemo kupooza.

Mahakama imetoa amri hiyo baada ya Didas kushinda kesi ya madai aliyoifungua dhidi ya taasisi hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii(wakati huo) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Itakumbukwa kuwa mwaka 2007 Didas alifanyiwa upasuaji wa kichwa alipofikishwa MOI badala ya mguu aliokuwa anaumwa. Mgonjwa mwenzake, Emmanuel Mgaya alifanyiwa upasuaji wa mguu ambao haukuwa na tatizo badala ya kichwaKutokana na makosa hayo, wagonjwa wote wawili walipelekwa katika hospitali ya Indraprastha Apollo, nchini India kwa matibabu zaidi hata hivyo, Mgaya alifariki dunia baadaye 

0 Comments

Previous Post Next Post