Alichokisema Mbowe Baada ya Sugu Kuachiwa.

Alichokisema Mbowe Baada ya Sugu Kuachiwa

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe amesema kwamba baada ya Sugu kuachiwa hatakwenda Bungeni moja kwa moja licha ya kwamba Bunge linaendelea, ila watamuacha arekebishe masuala yake ya kifamilia kwanza.


Mbowe ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na East Africa Radio, na kusema kwamba haitakuwa vyema kwa Mbunge huyo ambaye alikuwa akitumikia kifungo chake kumruhusu kwenda Bungeni mara moja, kwani ana mambo ya muhimu ya kushughulikia kwanza.

Sambamba na hayo Mbowe amesema alifika kwenye Gereza la Ruanda kumpokea Sugu akiwa na baadhi ya wanafamilia na viongozi wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, wakisubiria kukamilika kwa utaratibu wa kuachiwa huru kwa watu hao.

“Kwa vyovyote kwa mtu aliyekaa gerezani kwa siku zote hizi si rahisi kumtoa leo na kumpeleka Bungeni kesho, ila kwanza lazima mambo yake ya kifamilia yakitulia na mambo mengine akishayamaliza ndio tutaweza kujua ratiba ya Bunge inakuwaje, lakini ataweza kwenda Bungeni, hivi ninavyozungumza nipo mbele ya Gereza la Ruanda hapa Mbeyea, niko na kundi kubwa tu la viongozi Kanda ya Nyasa, wanafamilia na wanachama wa Chadema ambao wamekuja kuwapokea”, amesema Mbowe.

Sugu na Emmanuel Masonga walihukumiwa kifungo cha miezi mitano jela Februari 26, 2018, kwa kosa la kutoa lugha za kashfa. 

0 Comments

Previous Post Next Post