Yanga yawapa ilani waamuzi watakaochezesha Mechi dhidi ya Simba.

Uongozi wa klabu ya Yanga umewataka Waamuzi watakaochezesha mchezo wa kesho dhidi ya Simba kufuata sheria 17 za mchezo wa soka.

Kauli hiyo imetolewa na Yanga kupitia Afisa Habari wa timu hiyo, Dismas Teni, ambapo kikosi chao kitakuwa mgeni dhidi ya Simba.

Teni ameeleza kuwa timu zimewekeza kwenye mpira hivyo haitopendeza kuona Waamuzi wanaharibu ladha ya mpira na ksuhindwa kutafsiri sheria 17 za mchezo wa soka.

Timu hizo zinakutana kesho ikiwa ni katika mzunguko wa pili wa ligi, baada ya ule wa kwanza kwenda sare ya bao 1-1.

0 Comments

Previous Post Next Post