Wema atoa kali,siku ya mazishi yake.


HII ni kali! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya staa wa filamu Bongo, Wema Isac Sepetu, kutoa kali ya aina yake kwa kueleza namna mazishi yake yatakavyokuwa punde tu Mungu atakapoutwaa uhai wake.

Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya msanii mwingine wa Bongo Fleva na Bongo Movie, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kusema siku akifa, aagiwe msikitini na si kwingineko.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Wema alisema yeye angependa kwenye mazishi yake wahudhuriaji wapendeza, wafurahie maisha aliyokuwa akiishi na katika nyumba itakayokuwa na msiba wake, papambwe rangi ya pinki.

“Napenda sana siku ya mazishi yangu waombolezaji wawe kwenye muonekanao mzuri na pia sehemu ambayo mwili wangu utafikia pawe pamepambwa vizuri kwa maua ya pinki yanayovutia,” alisema Wema.

Staa huyo alifunguka zaidi kuwa kwenye mazishi yake hayo baada ya familia, mtu mwingine ambaye anataka awe mstari wa mbele kwenye mazishi yake ni staa mwenziye, Aunt Ezekiel na kudai kuwa yeye ndio ataweka ua wa kwanza kwenye kaburi lake kabla ya staa mwingine yeyote.

Wema alienda mbele zaidi na kusema kuwa kwa vile yeye ni mtoto wa Kiislam hatoruhusiwa kuagwa lakini jeneza lake lipambwe maua mengi ambapo watu watakuwa wamelizunguka na kuliombea.

“Ningependa sana baada ya familia yangu Aunt awe mstari wa mbele zaidi kuliko staa yeyote na yeye ndio aanze kuweka ua wa kwanza kwenye kaburi langu kabla ya staa yeyote yule na jeneza langu lipambwe maua mengi maana najua watu hawatoniaga,” alisema Wema.

0 Comments

Previous Post Next Post