Sir Alex Ferguson ampa Wenger zawadi maalum.


KOCHA wa zamani wa Klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson jana alimuaga Kocha wa Arsenal, Mzee Arsene Wenger kwa kumpa zawadi maalum kabla ya mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kati ya Arsenal na Man U.

Sir Alex Ferguson alimkabidhi zawadi hiyo maalum kwa niaba ya Klabu ya Manchester United ikiwa ni sehemu ya kutambua mambo mbalimbali ambayo Wenger ameyafanya kwenye Ligi Kuu ya Soka nchini Uingereza.

Mzee Wenger ambaye ameshatangaza rasmi kuachana na Arsenal ambayo ameitumikia kwa miaka 22 mwishoni mwa msimu huu licha ya kutoweka wazi iwapo atastaafu au atakwenda kufundisha klabu nyingine.

Katika mechi hiyo ya jana katika Uwanja wa Old Trafford, Man U waliichapa Arsenal kwa bao 2-1 huku mabao ya Man U yakifungwa na Paul Pogba  dakika ya 16 na Marouane Fellaini dakika ya 90 ambapo Arsenal lilifungwa na Henrikh Mikhtaryan dakika ya 51.

Wenger na Mourinho sasa wamekutana mara 13 na Mourinho ameshinda mara 8 na kutoka sare mara 5.

0 Comments

Previous Post Next Post