Mzee Majuto arudishwa Muhimbili,wiki ijayo kupelekwa India.


Msanii wa Filamu nchini, Mzee Majuto amerudishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo awali alikuwa akipatiwa matibabu kabla ya kuhamishiwa hopitali ya binafsi, Tumaini.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa serikali imeamua kumrudisha Hospitali ya Taifa ili kufanyiwa vipimo upya kujua kinachomsumbua.
“Wakati akisubiri kusafiri kwenda nje ya nchi (India) kati ya Jumatatu na Jumanne kwa ajili ya matibabu tumeamua tumuhamishie kwanza Muhimbili ili afanyiwe vipimo zaidi, lakini niwaambie mashabiki wake na Watanzania kwa ujumla kuwa Mzee Majuto anaendelea vizuri,” amesema Dkt. Mwakyembe.
Hapo jana April 27, 2018 Bungeni wakati ukiendelea mjadala wa bajeti ya
Wizari ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka 2018/19, Dkt. Mwakyembe alisema ameunda kamati ya wanasheria ili kupitia matangazo yote ya kibiashara aliyofanya msanii huyo ili kubaini iwapo anaibiwa kwani kwa sasa anategemea michango ili kufanikisha matibabu yake.

0 Comments

Previous Post Next Post