Mwameja ataja sababu iliyowaangusha Yanga.


Mlinda mlango wa zamani wa Simba, Mohamed Mwameja, ameeleza furaha yake kutokana na timu yake kuibuka na ushindi dhidi ya watani zao wa jadi, Yanga.

Mwameja aliyewahi kung'ara na kikosi hicho cha wekundu wa Msimbazi miaka ya nyuma na kujiwekea rekodi ya kuwa mmoja wa makipa bora kwenye soka la Tanzania hapa nchini, amefurahi ushindi huo akisema Simba walikuwa na kikosi kipana.

Mbali na furaha ya ushindi, Mwameja ametaja sababu iliyowaangusha Yanga dhidi ya Simba jina ni majeruhi walionao kwenye kikosi chao.

Kipa huyo wa zamani ameeleza kukosekana kwa baadhi ya wachezaji kama Donald Ngoma, Thaban Kamusoko, Amis Tambwe ambao ndiyo mhimili wa timu kumesababisha kikosi cha Yanga kuwa dhaifu kwenye mchezo wa jana.

0 Comments

Previous Post Next Post