Aslay akiri kifo cha Masogange ‘kupoteza’ ngoma yake


Msanii wa muziki Bongo, Aslay amesema ngoma yake ya mwisho kutoa ‘Kwa Raha’ licha kuendelea kufanya vizuri imekumbana na misukosuko.

Muimbaji huyo amesema ngoma hiyo aliitoa kama zawadi kwa mashabiki wake kwani ngoma yake ya mwisho kutoa rasmi ni Nibebe mara baada ya kubadilisha mfumo wake wa kutoa ngoma.
“Kwa Raha nilitoa kama zawadi kwa sababu kuna ngoma inakuja kuitoa tena baadaye ila nasema ni ngoma yangu naipenda na namshukuru Mwenyenzi Mungu imeenda japo kuwa hapa kati imekutana misukosuko, Agness amefariki, kuna vitu kibao vimetokea lakini nashukuru ngoma hivyo hivyo inaenda,” Aslay ameiambia Bongo5.
Ngoma ya Kwa Raha, Aslay aliitoa April 17, 2018, ngoma hiyo ambayo ni ya pili kwa yeye kutoa kwa mwaka huu hadi sasa ina views 481,993 katika mtandao wa YouTube.

0 Comments

Previous Post Next Post