Mama Kanumba Amtetea Hamissa Mobetto " Wote ni Watoto Wangu Hamisa Sio Mnafki"MAMA wa aliyekuwa nguli wa filamu Bongo marehemu Steven Kanumba,Flora Mtegoa amemkingia kifua mwanadada Hamisa Mobeto, baada ya mrembo huyo kuonekana mnafiki kwa kumsikitikia muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ kisha kuonekana akiwa beneti na mama huyo.

Hivi karibuni, Mobeto alionekana kwenye uzinduzi wa filamu ya Zero Player aliyoshirikiana na mdogo wa Kanumba, Seth Bosco akiwa na mama huyo ndipo watu mitandaoni walipoanza kumnanga kwa kumuita msaliti wakidai ni hivi karibuni tu, aliposti picha ya kumsikitikia Lulu aliyehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela ambaye hapatani na mama Kanumba.

Ishu hiyo ilimuibua mama Kanumba ambapo alimtetea Mobeto: “Sioni haja ya watu kumsema vibaya Hamisa, wote ni watoto wangu tatizo liko wapi, wasimuite mnafiki bwana,” alisema mama Kanumba. 

0 Comments

Previous Post Next Post