Kutana na Mwanamke Mnene Kuliko Wote Duniani… Ana Uzito wa Kilo 500

Kwa mujibu wa jarida la Daily Mail, inaelezwa kuwa mwanamke huyo aitwaye Iman Ahmad Abdulati mwenye miaka 36 hajawahi kutoka ndani kwa miaka 25 na amekua akiongezeka uzito wake kwa haraka mpaka kufikia kilo 500 zinazompa shida ya kujifanyia usafi na hata kula. Ripoti ya madaktari inaonesha kuwa mwanamke huyu anasumbuliwa na maambukizi ya bakteria wanaoshambulia ukuaji wa mwili. Akiwa na miaka 11 alianza kusumbuliwa na tatizo hilo ingawa wazazi wake wanakiri kuwa hawakudhani kuwa ni tatizo lakini siku zilivyozidi kwenda ndipo wakabaini kuwa halikua jambo la kawaida hivyo wakaamua kutafuta wataalamu ambao walitoa ripoti kuwa ana matatizo ya mwili wake kukaa na maji mengi bila kuyatoa nje kitu ambacho sio cha kawaida kwa binadamu.


0 Comments

Previous Post Next Post